KLABU ya simba imeendelea kuandamwa na majeruhi kuelekea kwenye mchezo wake dhidi ya Polisi Morogoro utakaofanyika Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salam majira ya saa kumi jioni.
Miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo ambao wamepata majeruhi ni Issa Rashid ''Baba ubaya'', Paulo Kiongera, Abdi Banda, Nassor Masoud chollo pamoja na mlinda mlango namba moja Ivo Mapunda.
Licha ya kuwa na majeruhi mengi hatutaraji kuona mapungufu mengi katika timu hiyo kwani ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kuziba mapengo hayo, hivyo jukumu kubwa linabaki kwa kocha wa timu hiyo pamoja benchi zima la ufundi kushauriana nani acheze katika nafasi hizo.
Tuliona katika mechi ya ufunguzi timu hiyo ilivyopoteza nafasi nyingi katika sehemu la umaliziaji kwani walikosa nafasi nyingi za kufunga magoli licha ya kuwa na safu hatari ya wafungaji huku ikiongozwa na mfungaji bora wa msimu uliopita Hamis Tambwe raia wa Burundi.
Habari njema kwa mashabiki klabu hiyo ni kurejea kwa kiungo mkabaji Jonas Mkunde aliye kuwa kwenye majeruhi kwa muda mrefu aliyopata akiwa katika kambi ya timu ya Taifa, hivyo ataongeza nguvu katika eneo la kati huku akisaidiana na mabeki wake.
Kwani katika mchezo uliopita tuliona mapungufu katika kiungo mkabaji hasa katika kipindi cha pili mpaka ikapelekea wapinzani kusawazisha magoli yote mawili licha ya kuongoza kipindi cha kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni