Jumanne, 30 Septemba 2014

HAPATOSHI LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA LEO JUMANNE

KIVUMBI kuendelea tena leo na kesho katika ligi ya mabingwa makundi mbalimbali kujaribu bahati zao na kutumia vizuri viwanja vya  nyumbani, mechi ya mapema itaanza majira ya saa moja usiku katika jiji la Moscow nchin Urusi kati ya mabingwa CSKA MOSCOW watavaana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.

Majira ya saa tatu na dakika arobaini na tano usiku makundi ya E na H yatawasha moto wakati wenyeji Manchester City wanawakarisha wageni As Roma toka Italia.

Macho na masikio yatakuwa kundi F katika jiji la Paris nchini Ufaransa mabingwa wa ligi hiyo Paris Saint Germain watakuwa wenyeji wa Fc Barcelona toka nchini Hispania kwani timu hizo zimekuwa na upinzani mkubwa kwani hata msimu uliopita  zilikuwa kundi moja ambapo mechi ya kwanza zilitoka sare na ziliporejeana Barcelona walishinda.
  Pia kutakuwa na mechi nyingine katika kundi hilo Apoel Nicosia na Ajax watavaana.

Vijana wa kupaki basi watakuwa nchini Ureno watakumbana na wenyeji  Sporting Lisbon timu ambayo haijafungwa katika mechi zake za ligi sawa na Chelsea nao hawajafungwa katika ligi ya England na Schalke 04 watawapokea Maribor katika kundi hilo la G.

Hitimisho la leo kundi H, Bate Borisov na Athletic Bilbao pamoja na Shakhtar Donetsk vs Fc Porto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni