Jumatano, 1 Oktoba 2014

ARSENAL NA MAJERUHI KUWAVAA WATURUKI LEO HII

PATASHIKA ya ligi ya mabingwa kuendelea leo hii baada ya kushudia vigogo toka Hispania timu ya Barcelona wakichezea kichapo cha magoli matatu toka kwa mabingwa wa Ufaransa timu ya Paris Saint Germain, Chelsea, Bayern Munich,wakipata ushindi wa ugenini na pia Manchester City wameendelea kuchechemea baada ya kulazimishwa sare na Roma toka Italia.

Je nani kuibeba Arsenal kwani kila siku majeruhi wanaongezeka baada ya kuona viungo wa timu hiyo kama Mikel Arteta, Aron Ramsey, Jack Wilshere watakosa mechi ya leo dhidi ya timu ya Galatasaray toka nchini Uturuki.Hivyo jukumu la kiungo mkabaji itawategemea Flamini, Diaby,Rosicky nani ataanza katika kikosi cha kwanza.


Hivyo kutakuwa na mabadiliko kwani namba nane atasimama Alex Oxlade-Chamberlain kulia na kushoto Mesut Ozil na Alexis Sanchez wataongoza kutoa pasi kwa Santi Cazorla na Dany Welbeck huu utakuwa mtihani mgumu kwa Asener Wenger kwani mwishoni mwa wiki atakuwa ugenini kupepetana na watoto wa kupaki basi Chelsea ambao mpaka sasa hawajafungwa katika ligi ya England .

Mechi nyingine
Atletico Madrid vs Juventus,
Fc Basel             vs Liverpool
Malmo               vs  Real Madrid


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni