Ijumaa, 24 Oktoba 2014

DUNIA ITASIMAMA KWA DAKIKA 90 USIKU WA EL CLASSICO


DUNIA itasimama kwa muda wa dakika tisini  majira ya saa moja kamili usiku pale mahasimu wa soka nchini Hispania  Barcelona na Real Madrid  katika mechi ya la liga, upinzani uliopewa jina la El Classico na pia zikipambwa na majina makubwa ya wanasoka wenye upinzani mkubwa kwa soka la sasa  Messi na Ronaldo.

Upinzani utaongezeka kwa pande zote mbili kwani kila timu imesajili wachezaji wapya, macho na masikio ni kwa nyota mpya wa timu ya Barcelona Luis Suerez,  kwa mara ya kwanza ataonekana katika timu yake. Baada ya kumaliza kifungo cha miezi minne baada ya kumnga'ta  mchezaji wa timu ya Taifa ya Italia  la katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil.

Kwa upande wa mechi yenyewe itakuwa ngumu kwa kila upande kwani  sasa timu ya Barcelona haijafungwa na pia haijaruhusu goli lolote katika michezo minane ya ligi hiyo na kujikusanyia point ishirini na mbili imeshinda saba na kutoka sare moja. Na mahasimu wao wana point kumi na nane wamefungwa mechi moja na kutoka sare moja.

Macho ya wengi ni kwa wachezaji wa timu hizo Lionel Mess, Christian Ronaldo ndio wanatazamwa kwa kila mtu kutokana na ubora walio nao kwa sasa japo kuwa Ronaldo anaongoza kwa kupachika magoli kwa ligi hiyo ana magoli kumi na tano na mpinzani wake ana magoli saba.

Je Luiz Suerez ataanza vyema kwa timu yake kwa kushirikiana na nyota aliye kwenye kiwango cha juu kwa sasa na ndie anaongoza kwa kupachika magoli katika klabu yake Junior Santos Nermar pingo kubwa litakuwa kwa Real Madrid kwa kumkosa winga wao hatari aliye majeruhi Gareth Bale.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni