Jumatatu, 27 Oktoba 2014

SIMBA SASA HALI YAZIDI KUWA TETE

SARE,ya tano mfululizo katika klabu ya Simba imewachanganya viongozi pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Phiri na benchi lake la ufundi,  mpaka kufikia hatua ya kuwatuhumu baadhi ya wachezaji wa timu hiyo akiwemo Amri Kiemba na Haruna Chanongo kuwa hawajitumi ipasavyo.

Kwa kawaida matokea ya timu hiyo ni mazuri kwani mpaka sasa haijafungwa katika ligi ya Vodacom Tanzania Bara kufungwa,sare na kupata point ni moja ya matokeo ya mpira wa mguu kwa hali inavyoendelea. Kunaelekea katika timua timua ya kocha,wachezaji kutuhumiwa kuwa wanahujumu timu kwani ndio ilivyo katika klabu zetu kongwe hapa nchini  zenye viongozi walioathirika kimawazo.

Tujiulize nani wa kulaumiwa katika timu hiyo kati ya  wachezaji na kocha? ama uongozi wenyewe ukae chini ujiulize nani mchawi wa sare tano kwa upande wangu naona ndani ya uongozi kuna matatizo,  kuna kundi la Ukawa ambalo limefutwa uanachama kuwa waliipeleka Simba Mahakamani katika kipindi cha Uchaguzi uliopita.

Kwanini nasema kuwa kuna matatizo katika timu hiyo ni kuwa baadhi ya wachezaji wameanza kutuhumiwa kuwa wanahujumu timu kwa mjibu wa kiongozi moja wa timu hiyo,  amefikia hatua ya kusema katika chombo kimoja cha habari kuwa, Amri Ramadhani Kiemba  anahujumu timu kwa kucheza chini ya kiwango akiwa kwenye timu ya Taifa Star anacheza kwa kujituma.?

Kweli kwa hali ilivyo Kiongozi kuanza  kumtuhumu mchezaji kwa kuangalia kocha Phiri hampi nafasi kubwa  ya kucheza na kwenye kikosi chake huku  timu ya Taifa anaaminiwa na kocha mkuu. Sasa kiongozi huyo ana ushahidi gani kuwa mchezaji huyo  anahujumu timu? basi angejaribu japo kutumia busara ya kuzungumza na wachezaji anaowahisi wanaihujumu timu kwanza  au hata kundi linalijiita Ukawa pamoja na Baraza la Wazee wa timu hiyo ambao wanaonekana kutengwa na Uongozi na sio kuwanyoshea kidole wachezaji.

Huo unaonekana kuwa mwanzo tu lakini inawezekana zengwe hili litamkuta  hata kocha mkuu wa  wa timu hiyo kwani baada ya kutoka sare na Prison ya mkoani Mbeya  kuna mambo mengi yatatokea katika timu likiwemo la  kusimamishwa kwa wachezaji kumkalisha kitimoto kocha mkuu na benchi lake la ufundi. Kwa matokeo mabaya yanayoikumba klabu hiyo usije kushangaa kuona Kiemba,Shabani Kisinga na Haruna Chanongo wamesimamishwa kwa kutuhumiwa kwa kuhujumu timu.

Hivyo tunachoomba wana msimbazi waendelee kuwaamini wachezaji na sio kuanza kutuhumu kwa mambo ya siasa kwani tatizo wanalo wenyewe cha kuwashauri wakae chini na Ukawa na Wazee wa klabu hiyo,  ili watatue matatizo ya timu na wala sio kuwalaumu wachezaji. Tunajua kuwa Simba ina Rais anayejua mpira Evans Aveva atumie busara kutatua mgogoro uliopo ndani ya timu maana inavyoelekea mambo yataendelea kuwa magumu kupita maelezo.

itaendelea wiki ijayo


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni