Jumatatu, 6 Oktoba 2014

LIGI  ya Vodacom Tanzania bara ipo katika mzunguko wa tatu tumeshudia timu mbalimbali zikiendeleza ushindi nyingine sare pamoja na kufungwa hayo yote ni matokeo ya mpira kwani kuna kushinda,sare na kufungwa.

Je tutafika katika kukuza mpira wa Tanzania tuwe kama  nchi  nyingine barani Afrika ama Ulaya? kwani mpaka sasa kuna mvutano baina ya TFF na timu zinazoshiriki katika ligi hiyo shirikisho linalosimamia mpira tayari limesema lazima kila timu ikatwe asilimia tano ya wadhamini wa ligi.

Ambao ni Vodacom pamoja na Azam Media kwani ndio wadhamini wa ligi hiyo kwa mjibu wa TFF wamesema wameazisha mfuko wa maendeleo ya timu za vijana na mapato yake yatapatikana kutokana na makato ya vilabu vinavyoshiriki ligi ya Vodacom je huu ni mfumo sahihi kwa shirikisho hilo chini ya Rais Jamal Malinzi vimezingatia hali halisi iliyopo katika timu zinazoungaunga kupata hela?

Kuna haja gani vilabu vikatwe mapato kama hayo kwanini TFF isibuni njia nyingine ya kupata hizo pesa za kuendeshea vijana mpaka isake mapato kwa timu hizo huu ni mgogoro mkubwa mno kwani kila upande ukimtunishia  misuri mwenzake na tayari Malinzi kasema lazima kila timu ikatwe asilimia tano huku mwanasheria wa vilabu hivyo Damasi Ndumbaro amesema haiwezekani kukatwa asilimia hiyo.

Je timu kama Stand United ,Ndanda Fc, Coast Union, ambazo zinapata hela kutoka kwa kutembeza bakuli kwa watu zitaweza kweli kuwalipa mishahara wachezaji na benchi zima la ufundi mpaka leo hii vilabu vinalia pesa haitoshi kwa mahitaji ya timu haki imetendeka ama shirikisho hilo limekurupuka kwa maamuzi hayo kwa vilabu.

Kwa hili naona TFF hawajatenda haki kwa kuamua kuingia kwenye mvutano ambao hauna maana kwa kuendesha mpira wa miguu wangebuni kitu kingine cha kuwaingizia mapato bila wasiwasi mfano mzuri wangeandaa semina kwa wadau wa mpira na pia wangeandaa mechi maalum kwa timu ya Taifa kwa lengo kupata hizo pesa na pia wangetafuta wadhamini.

Kwa ushauri wangu kwa shirikisho hilo liache kutumia nguvu kwa vilabu hivyo bali litumie vyanzo vingine kwa kuendeshea mfuko huu ambao wameanzisha na sio kwa kuzizamisha timu mpaka ikapelekea kuvurungika kwa ligi hiyo, maana tunapoelekea mambo mengi yataendelea kutokea.

Hivyo busara itumike kwa maamuzi hayo hatupendi kuona soka letu likiendelea kuwa chini badala ya kufikiri mbele kwani sisi tunazozana na makato ya pesa wenzetu wanafikiria maandalizi ya kombe la Dunia mwaka 2018 litakalo fanyika nchini Urusi.

















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni