Alhamisi, 2 Oktoba 2014
ARSENAL BILA KUPEPESA MACHO WAPELEKA MSIBA MZITO UTURUKI.
WASHIKA,bunduki wa Jiji la Kaskazini mwa London timu ya Arsenal kuamkia usiku wa Ulaya jana wamefanya mauaji makubwa dhidi ya wahuni wa Uturuki timu ya Galatasaray kwa kuwafunga magoli manne kwa moja.
Iliwachukua dakika ya ishirini na mbili kipindi cha kwanza mshambuliaji hatari aliye sajiliwa katika dakika za majeruhi toka kwa wapinzani wao Manchester United Dany Welback aliipatia goli la kwa baada ya kupokea pasi zuri toka kwa Alexis Sanchez ,dakika 30 aliweka nyavuni goli la pili safari hii akiwahi pasi ya Mesut Ozil kabla ya kwenda mapumziko Alexis Sanchez alihitimisha goli la tatu.
Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliana kwa zamu huku wageni wakitafuta kurejesha magoli yote waliofungwa kipindi cha kwanza dakika ya hamsini Welback aliandika hat trick yake ya kwanza akiwa na Arsenal na pia ni goli lake la nne tangu ajiunge na timu hiyo.
Mshambuliaji huyo aliyekuwa mwiba kwa kuisumbua ngome ya wapinzani hao huku Felipe Melo akizungushwa na Sanchez pamoja mabeki wake dakika ya 69 washika bunduki hao walipata pigo baada ya mlinda mlango Szczesny kupata kandi nyekundu kwa kosa la kumdaka mshambuliaji wa Galatasaray.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni