Mzunguko roundi ya tano wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara kuendelea tena mwishoni mwa wiki hii katika viwanja tofauti tofauti macho na masikio ya wengi yatakuwa katika viwanja vya Kambarage mjini Shinyanga na Sokoine mjini Mbeya huku vigogo vya Simba na Yanga vitakuwa ugenini.
Mechi nyingine mabingwa watetezi wa ligi hiyo Azam FC watakuwa nyumbani kuwaalika watoto waliokuwa usingizini Jkt Ruvu katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salamu huku watoto wa Mabati Pwani Ruvu shooting mara baada ya kuzinduka mpaka kupelekea kufukuzwa kwa kocha wa Ndanda FC watakuwa nyumbani kupepetana na Polisi Morogoro,wagonga nyundo Mbeya City baada ya kupokea kichapo toka kwa Azam watakuwa nyumbani kuwapokea vijana toka kwenye mashamba ya Miwa Mtibwa Sugar.
Je Simba atavunja mwiko dhidi ya Tanzania Prison katika uwanja wa Sokoine ambao umekuwa mgumu mno kwa wekundu wa msimbazi mara nyingi tumeshudia wakichezea vichapo ama kutoka sare Simba hawana bahati katika viwanja vya mikoani kwani hata msimu uliopita walipata point tatu tu katika mechi za ugenini nyingi walitoka sare pamoja na kufungwa ushindi wao ulikuwa katka uwanja wa Sheik Abedi Karume mjijini Arusha dhidi ya Jkt Oljoro.
Watoto wa Marcio Maximo watakuwa wageni wa timu mpya iliyo panda ligi kuu kwa mara ya kwanza Stand United ambayo mpaka sasa haijapoteza mechi yeyote ya ugenini kwani imeweza kupata pointi tano japo ilianza vibaya katika uwanja wake wa nyumbani kwa kufungwa magoli manne kwa moja na Ndanda FC,je watakuwa wateja katika uwanja wake dhidi ya timu ya Yanga?
Mara nyingi tumeshudia timu za Simba na Yanga zinapocheza ugenini huwa zinakabiwa mno na timu pinzani kutokana na kuwa na majina makubwa katika soka la Tanzania mambo mengi hutokea katika mechi hizo ushirikina mara nyingi hutokea mfano msimu uliopita mjini Tanga mchezo baina Jkt Mgambo naTimu ya Yanga na Mbeya City na Simba mjini Mbeya mambo hayo ya ushirikina yalitokea katika viwanja vingi ambapo Simba na Yanga zinapokuwa ugenini.
Kwa muda mrefu wakazi wa mjini Shinyanga hawakuwa na timu kwa takribani miaka kumi hawazioni timu za Simba naYanga baada ya timu yao iliposhuka daranja Kahama Unitedi hajawahi tena kuona uwanja wao ukitumika tunajua jumamosi mechi itakuwa kali na kusisimu kwa timu zote mbili na pia uwanja utafurika mno hii kutokana na watu wengi wa kanda ya ziwa kuwa hamasa ya mpira.
Hivyo tunatarajia kuwa mechi yote itakuwa migumu kutokana na kila timu zimejipanga vya kutosha katika safari ya kutafuta pointi tatu muhimu kwa kila timu wasimamzi,wamzi tunawaomba wafate sheria zote za mpira wa miguu hatutaki kuona wakipendelea timu fulani pamoja na timu zitakapofungwa mara nyingi tumeona makocha huwa wanalalamika pindi timu zinapofungwa utasikia refa kapendelea timu fulani ama viwanja vibovu yote hayo hutokea mara tu dakika tisini za mwamuzi zinapoisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni