SARE,ya tano mfululizo katika klabu ya Simba imewachanganya viongozi pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Phiri na benchi lake la ufundi, mpaka kufikia hatua ya kuwatuhumu baadhi ya wachezaji wa timu hiyo akiwemo Amri Kiemba na Haruna Chanongo kuwa hawajitumi ipasavyo.
Kwa kawaida matokea ya timu hiyo ni mazuri kwani mpaka sasa haijafungwa katika ligi ya Vodacom Tanzania Bara kufungwa,sare na kupata point ni moja ya matokeo ya mpira wa mguu kwa hali inavyoendelea. Kunaelekea katika timua timua ya kocha,wachezaji kutuhumiwa kuwa wanahujumu timu kwani ndio ilivyo katika klabu zetu kongwe hapa nchini zenye viongozi walioathirika kimawazo.
Tujiulize nani wa kulaumiwa katika timu hiyo kati ya wachezaji na kocha? ama uongozi wenyewe ukae chini ujiulize nani mchawi wa sare tano kwa upande wangu naona ndani ya uongozi kuna matatizo, kuna kundi la Ukawa ambalo limefutwa uanachama kuwa waliipeleka Simba Mahakamani katika kipindi cha Uchaguzi uliopita.
Kwanini nasema kuwa kuna matatizo katika timu hiyo ni kuwa baadhi ya wachezaji wameanza kutuhumiwa kuwa wanahujumu timu kwa mjibu wa kiongozi moja wa timu hiyo, amefikia hatua ya kusema katika chombo kimoja cha habari kuwa, Amri Ramadhani Kiemba anahujumu timu kwa kucheza chini ya kiwango akiwa kwenye timu ya Taifa Star anacheza kwa kujituma.?
Kweli kwa hali ilivyo Kiongozi kuanza kumtuhumu mchezaji kwa kuangalia kocha Phiri hampi nafasi kubwa ya kucheza na kwenye kikosi chake huku timu ya Taifa anaaminiwa na kocha mkuu. Sasa kiongozi huyo ana ushahidi gani kuwa mchezaji huyo anahujumu timu? basi angejaribu japo kutumia busara ya kuzungumza na wachezaji anaowahisi wanaihujumu timu kwanza au hata kundi linalijiita Ukawa pamoja na Baraza la Wazee wa timu hiyo ambao wanaonekana kutengwa na Uongozi na sio kuwanyoshea kidole wachezaji.
Huo unaonekana kuwa mwanzo tu lakini inawezekana zengwe hili litamkuta hata kocha mkuu wa wa timu hiyo kwani baada ya kutoka sare na Prison ya mkoani Mbeya kuna mambo mengi yatatokea katika timu likiwemo la kusimamishwa kwa wachezaji kumkalisha kitimoto kocha mkuu na benchi lake la ufundi. Kwa matokeo mabaya yanayoikumba klabu hiyo usije kushangaa kuona Kiemba,Shabani Kisinga na Haruna Chanongo wamesimamishwa kwa kutuhumiwa kwa kuhujumu timu.
Hivyo tunachoomba wana msimbazi waendelee kuwaamini wachezaji na sio kuanza kutuhumu kwa mambo ya siasa kwani tatizo wanalo wenyewe cha kuwashauri wakae chini na Ukawa na Wazee wa klabu hiyo, ili watatue matatizo ya timu na wala sio kuwalaumu wachezaji. Tunajua kuwa Simba ina Rais anayejua mpira Evans Aveva atumie busara kutatua mgogoro uliopo ndani ya timu maana inavyoelekea mambo yataendelea kuwa magumu kupita maelezo.
itaendelea wiki ijayo
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Makala. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Makala. Onyesha machapisho yote
Jumatatu, 27 Oktoba 2014
Alhamisi, 23 Oktoba 2014
MZUNGUKO ROUNDI YA TANO LIGI YA VODACOM TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII SIMBA NA YANGA UGENINI?
Mzunguko roundi ya tano wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara kuendelea tena mwishoni mwa wiki hii katika viwanja tofauti tofauti macho na masikio ya wengi yatakuwa katika viwanja vya Kambarage mjini Shinyanga na Sokoine mjini Mbeya huku vigogo vya Simba na Yanga vitakuwa ugenini.
Mechi nyingine mabingwa watetezi wa ligi hiyo Azam FC watakuwa nyumbani kuwaalika watoto waliokuwa usingizini Jkt Ruvu katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salamu huku watoto wa Mabati Pwani Ruvu shooting mara baada ya kuzinduka mpaka kupelekea kufukuzwa kwa kocha wa Ndanda FC watakuwa nyumbani kupepetana na Polisi Morogoro,wagonga nyundo Mbeya City baada ya kupokea kichapo toka kwa Azam watakuwa nyumbani kuwapokea vijana toka kwenye mashamba ya Miwa Mtibwa Sugar.
Je Simba atavunja mwiko dhidi ya Tanzania Prison katika uwanja wa Sokoine ambao umekuwa mgumu mno kwa wekundu wa msimbazi mara nyingi tumeshudia wakichezea vichapo ama kutoka sare Simba hawana bahati katika viwanja vya mikoani kwani hata msimu uliopita walipata point tatu tu katika mechi za ugenini nyingi walitoka sare pamoja na kufungwa ushindi wao ulikuwa katka uwanja wa Sheik Abedi Karume mjijini Arusha dhidi ya Jkt Oljoro.
Watoto wa Marcio Maximo watakuwa wageni wa timu mpya iliyo panda ligi kuu kwa mara ya kwanza Stand United ambayo mpaka sasa haijapoteza mechi yeyote ya ugenini kwani imeweza kupata pointi tano japo ilianza vibaya katika uwanja wake wa nyumbani kwa kufungwa magoli manne kwa moja na Ndanda FC,je watakuwa wateja katika uwanja wake dhidi ya timu ya Yanga?
Mara nyingi tumeshudia timu za Simba na Yanga zinapocheza ugenini huwa zinakabiwa mno na timu pinzani kutokana na kuwa na majina makubwa katika soka la Tanzania mambo mengi hutokea katika mechi hizo ushirikina mara nyingi hutokea mfano msimu uliopita mjini Tanga mchezo baina Jkt Mgambo naTimu ya Yanga na Mbeya City na Simba mjini Mbeya mambo hayo ya ushirikina yalitokea katika viwanja vingi ambapo Simba na Yanga zinapokuwa ugenini.
Kwa muda mrefu wakazi wa mjini Shinyanga hawakuwa na timu kwa takribani miaka kumi hawazioni timu za Simba naYanga baada ya timu yao iliposhuka daranja Kahama Unitedi hajawahi tena kuona uwanja wao ukitumika tunajua jumamosi mechi itakuwa kali na kusisimu kwa timu zote mbili na pia uwanja utafurika mno hii kutokana na watu wengi wa kanda ya ziwa kuwa hamasa ya mpira.
Hivyo tunatarajia kuwa mechi yote itakuwa migumu kutokana na kila timu zimejipanga vya kutosha katika safari ya kutafuta pointi tatu muhimu kwa kila timu wasimamzi,wamzi tunawaomba wafate sheria zote za mpira wa miguu hatutaki kuona wakipendelea timu fulani pamoja na timu zitakapofungwa mara nyingi tumeona makocha huwa wanalalamika pindi timu zinapofungwa utasikia refa kapendelea timu fulani ama viwanja vibovu yote hayo hutokea mara tu dakika tisini za mwamuzi zinapoisha.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)