Jumamosi, 4 Oktoba 2014

YANGA KUIBANA MBAVU RUVU JKT UWANJA WA TAIFA


MAKALI ya timu ya Yanga kuendelea kwa wanajeshi Jkt Ruvu katika mzunguko wa tatu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara. Huku kila timu ikitafuta point tatu muhimu huku vijana wa Fred Minziro wakitafuta ushindi wa kwanza kwani wametoka sare moja dhidi ya Mbeya City pamoja na kufungwa na mabingwa watetezi Azam Fc.

Hivyo kwa siku ya kesho tutaona mechi itakuwa ngumu kwa pande zote mbili,  Yanga iliyo chini ya kocha Mbrazil Marcio Maximo ikitaka kuendeleza ushindi wa pili baada ya kuifunga Tanzania Prisons kwani mechi ya kwanza walifungwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro magoli mawili kwa bila katika uwanja wa Jamhuri.

Je Andrey Coutinho ataendelea kuwatesa mabeki wa timu pinzani?  kwani tuliona katika mechi yake ya kwanza ya ligi alionyesha kazi na ufundi wa kuuchezea mpira, hali iliyopelekea kufunga goli zuri kwa njia ya faulo huku akiwa ametoka kwenye majeruhi yaliyomfanya akose mechi ya ufunguzi.

Hata hivyo upinzani utakuwa mkali kwa kuwa kocha Minziro anawafahamu vizuri Yanga alishawahi kuwafundisha Yanga,  swali la kujiuliza atakubali kufungwa na Maximo ama atapeleka msiba jangwani?  hilo ni swali ambalo kitendawili kitajibiwa  katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salamu.

Kwa kawaida mabeki wa Jkt Ruvu watakuwa na kazi ngumu kwani timu ya Yanga ina washambuliaji,viungo pamoja na mawinga wenye kasi  akili yakupiga mipira mifupi mifupi. Hivyo Ruvu wataingia kwa kukamia mechi wakitambua wazi kuwa watakutana na aina ya wachezaji wajanjahali itakayowaathiri kama ilivyokuwa kwa Prisons 

Kasi, nguvu na akili za winga machachari  Mrisho Ngasa,Simoni Msuva pamoja na wabrazil Coutinho na Jaja zinaweza kutosha kupeleka msiba mkubwa kwa Ruvu JKT wasipotambua nini wanapaswa kukifanya kwa wanajangwani hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni