KISASI timu ya Real Madrid toka nchini Hispania usiku wa kuamkia leo imetoka kifua mbele baada ya kulipa kisasi cha mwaka 2008 cha kufungwa magolin manne kwa moja mshambuliaji aliye kwenye kiwango cha Dunia Christian Ronaldo ameendelea kucheka na nyavu za wapinzani baada ya kufungwa goli la kwanza na magoli mawili yakifungwa na Karim Benzema yote yakipatikana kipindi cha kwanza.
Matokeo mengine Atletico Madridi wakiwaangamiza Malmo FC magoli matano kwa bila,huko nchini Uturuki vibonde Galatasaray wameendelea kugawa point baada ya kufungwa magoli manne kwa bila na vibonde wa ligi ya Ujerumani Borrusia Dotmund ambao mpaka sasa hawajafungwa goli lolote kwenye kundi hilo.
Arsenal wamepata ushindi wao kwa taabu baada ya kuwafunga Anderlecht magoli mawili kwa moja nchini Ufaransa Monaco wakitoka sare ya bila kufungana na Benfica huko kibibi kizee Juventus toka nchini Italia wakipokea kichapo toka kwa Olimpiakos kwa goli moja kwa bila.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni