LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara imeendelea tena wikiendi hii huku michezo kadhaa ikipigwa katika viwanja vitano tofauti lakini kubwa zaidi ni ile mechi kati ya Simba na Stand United iliyochezwa uwanja wa taifa Dar Es Salaam ikishuhudiwa Simba ikilazimishwa tena sare ya goli moja kwa moja.
Hii ni sare ya tatu kwa timu ya Simba tangu ligi kuu ianze na hivyo imepata pointi tatu na magoli manne katika michezo mitatu walioicheza tena katika uwanja mmoja wa taifa, hali inayoonesha kuwa bado haijajipanga vizuri kukabiliana na mikikimikiki ya ligi kuu inayoonekana kuwa ngumu kwa timu zote kucheza kwa juhudi kuhakikisha wanavuna pointi tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania kombe hilo.
Kuna mambo ambayo huibuka pindi hizi timu kongwe kama Simba inapozidiwa na kutoa matokeo ya aina kama hii kuwa inawezekana kuna tatizo, huku wakisahau kuwa mchezo ni mabadiliko na kila timu inafanya jitihada kubwa kuhakikisha inavuna pointi tatu. Hivyo matokeo wanayoyapata ni ya kawaida sana kutokana na ukweli kuwa kwa sasa dunia imebadilika na kila timu imebadilika na inafanya kila mbinu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Hivyo ni bora wapenzi na wadau wa soka wakaelewa kuwa mpira hausimami katika umbo lilelile bali hubadilika kulingana na wakati na namna dunia inavyoendelea, kinachotakiwa kwa timu ya simba ni kuhakikisha wanabaini nini kinawakwamisha kupata ushindi ili kujikwamnua na hali hii inayoonekana kuwakatisha tamaa mashabiki wa timu hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni