USIKU wa ulaya kuendelea leo hii katika viwanja tofauti tofauti swali la kujiuliza nani atavuna idadi kubwa ya magoli kama mechi za jana kwani magoli 40 yalipatikana huku Bayern Munich na Shakhtar Donestik zikifanya mauaji ya kutosha kwani ziliweza kushinda kwa idadi kubwa ya magoli.
Macho na masikio yatakuwa nchini England majogoo wa Anfield Liverpool watakuwa wanapepetana na mabingwa watetezi wa kombe hilo Real Madrid toka Hispania huo utakuwa mchezo mkali na wa kuvutia kwa timu zote mbili kwani zinapokutana huwa zina upinzani mkubwa mno.
Je Liverpool wataendeleza ubabe kwa mabingwa hao ama Madrid watalipa kisasi cha magoli manne waliofungwa katika mechi ya mwisho kukutana mwaka 2008\09 katika mchezo wa kwanza Liverpool alishinda goli moja kwa bila na ziliporejeana kwa mara nyingine Liverpool alishinda magoli manne kwa moja.
Mechi nyingine watoto wa kaskazini mwa London timu ya Arsenal watakuwa ugenini nchini Ubelgiji kupepetana na Anderlecht,Nchini Ufaransa matajiri Monaco wanaochechemea katika ligi ya kwao watawapokea vijana toka Ureno Benfica, vibonde toka Ujerumani Borrusia Dotmund watakuwa ugenini na wahuni wa Uturuki Galastaray,Atletico Madrid watakuwa nyumbani na Malmo FC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni