Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uchambuzi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uchambuzi. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 6 Oktoba 2014

LIGI  ya Vodacom Tanzania bara ipo katika mzunguko wa tatu tumeshudia timu mbalimbali zikiendeleza ushindi nyingine sare pamoja na kufungwa hayo yote ni matokeo ya mpira kwani kuna kushinda,sare na kufungwa.

Je tutafika katika kukuza mpira wa Tanzania tuwe kama  nchi  nyingine barani Afrika ama Ulaya? kwani mpaka sasa kuna mvutano baina ya TFF na timu zinazoshiriki katika ligi hiyo shirikisho linalosimamia mpira tayari limesema lazima kila timu ikatwe asilimia tano ya wadhamini wa ligi.

Ambao ni Vodacom pamoja na Azam Media kwani ndio wadhamini wa ligi hiyo kwa mjibu wa TFF wamesema wameazisha mfuko wa maendeleo ya timu za vijana na mapato yake yatapatikana kutokana na makato ya vilabu vinavyoshiriki ligi ya Vodacom je huu ni mfumo sahihi kwa shirikisho hilo chini ya Rais Jamal Malinzi vimezingatia hali halisi iliyopo katika timu zinazoungaunga kupata hela?

Kuna haja gani vilabu vikatwe mapato kama hayo kwanini TFF isibuni njia nyingine ya kupata hizo pesa za kuendeshea vijana mpaka isake mapato kwa timu hizo huu ni mgogoro mkubwa mno kwani kila upande ukimtunishia  misuri mwenzake na tayari Malinzi kasema lazima kila timu ikatwe asilimia tano huku mwanasheria wa vilabu hivyo Damasi Ndumbaro amesema haiwezekani kukatwa asilimia hiyo.

Je timu kama Stand United ,Ndanda Fc, Coast Union, ambazo zinapata hela kutoka kwa kutembeza bakuli kwa watu zitaweza kweli kuwalipa mishahara wachezaji na benchi zima la ufundi mpaka leo hii vilabu vinalia pesa haitoshi kwa mahitaji ya timu haki imetendeka ama shirikisho hilo limekurupuka kwa maamuzi hayo kwa vilabu.

Kwa hili naona TFF hawajatenda haki kwa kuamua kuingia kwenye mvutano ambao hauna maana kwa kuendesha mpira wa miguu wangebuni kitu kingine cha kuwaingizia mapato bila wasiwasi mfano mzuri wangeandaa semina kwa wadau wa mpira na pia wangeandaa mechi maalum kwa timu ya Taifa kwa lengo kupata hizo pesa na pia wangetafuta wadhamini.

Kwa ushauri wangu kwa shirikisho hilo liache kutumia nguvu kwa vilabu hivyo bali litumie vyanzo vingine kwa kuendeshea mfuko huu ambao wameanzisha na sio kwa kuzizamisha timu mpaka ikapelekea kuvurungika kwa ligi hiyo, maana tunapoelekea mambo mengi yataendelea kutokea.

Hivyo busara itumike kwa maamuzi hayo hatupendi kuona soka letu likiendelea kuwa chini badala ya kufikiri mbele kwani sisi tunazozana na makato ya pesa wenzetu wanafikiria maandalizi ya kombe la Dunia mwaka 2018 litakalo fanyika nchini Urusi.

















Jumatatu, 29 Septemba 2014

MZIMU WA MSOTI WAENDELEA KUITESA SIMBA

TIMU ya Simba imeendelea kupata sare ya pili mfululizo katika mechi za ligi ya Vodacom Tanzania Bara huku tukiona uwezo wa kila mchezaji anayepata nafasi katika kikosi cha kwanza kati ya wachezaji wote waliosajiliwa na timu hiyo.

Licha ya kuwa na wachezaji wenye viwango vya kimatifa na wenye uzoefu katika mashindano mbalimbali hatujaona makali yao kama vile, kurejea kwa kiungo mkabaji Jonas Mkude hatujaona msaada mkubwa kuwalinda mabeki wake kwani timu hiyo inakosa pumzi katika kipindi cha pili.

Tatizo kubwa ambalo ni changamoto kwa kocha Patriki Phiri na bechi lake la ufundi ni sehemu ya mabeki wake kwani kumekuwa hakuna uwiano mzuri kati ya beki wa mwisho na wa nyuma bado kuna leta shida sana katika ukabaji wake,je nani tumlaum kocha aliyemuacha Donald Musoti ama kamati ya usajili iliyoamua kumsajili Emanueli Okwi?

Kwa upande wangu mzimu wa Musoti utaendelea kuitesa timu hiyo, kwani  ndio alikuwa nguzo imara katika ulinzi akisaidiana na Josefu Owino katika msimu uliopita, ushirikiano wao ulionekana hasa kwenye mechi ya mtani jembe walivyoweza kuwadhibiti washambuliaji wa timu ya Yanga

 Je kulikuwa na haja gani ya kumuacha beki kisiki na kuamua kumrudisha Okwi? ama ndio soka la Usimba na Uyanga wa kukomoana katika suala zima la usajili, wa timu hizi mbili zenye washabiki wengi nchini,ama siasa nyingi na majingambo mengi ambayo hayasaidii katika kujenga timu.

Musoti ni beki wa kimataifa na ana uwezo mkubwa sana katika ukabaji leo hii anaachwa na hatukuona nafasi yake anasajiliwa beki mzoefu  kwa lengo la kuziba nafasi yake. Isihaka bado hajawa na uzoefu katika mikikimiki ya mechi mbalimbali, wadau wengi bado wanajiuliza maswali je ni kocha hakuridhika na kiwango cha mchezaji huyo ama kamati ya usajili kwa ajili ya kufurahisha mashabiki wake na uongozi mpya uliopo sasa?