TIMU ya Simba imeendelea kupata sare ya pili mfululizo katika mechi za ligi ya Vodacom Tanzania Bara huku tukiona uwezo wa kila mchezaji anayepata nafasi katika kikosi cha kwanza kati ya wachezaji wote waliosajiliwa na timu hiyo.
Licha ya kuwa na wachezaji wenye viwango vya kimatifa na wenye uzoefu katika mashindano mbalimbali hatujaona makali yao kama vile, kurejea kwa kiungo mkabaji Jonas Mkude hatujaona msaada mkubwa kuwalinda mabeki wake kwani timu hiyo inakosa pumzi katika kipindi cha pili.
Tatizo kubwa ambalo ni changamoto kwa kocha Patriki Phiri na bechi lake la ufundi ni sehemu ya mabeki wake kwani kumekuwa hakuna uwiano mzuri kati ya beki wa mwisho na wa nyuma bado kuna leta shida sana katika ukabaji wake,je nani tumlaum kocha aliyemuacha Donald Musoti ama kamati ya usajili iliyoamua kumsajili Emanueli Okwi?
Kwa upande wangu mzimu wa Musoti utaendelea kuitesa timu hiyo, kwani ndio alikuwa nguzo imara katika ulinzi akisaidiana na Josefu Owino katika msimu uliopita, ushirikiano wao ulionekana hasa kwenye mechi ya mtani jembe walivyoweza kuwadhibiti washambuliaji wa timu ya Yanga
Je kulikuwa na haja gani ya kumuacha beki kisiki na kuamua kumrudisha Okwi? ama ndio soka la Usimba na Uyanga wa kukomoana katika suala zima la usajili, wa timu hizi mbili zenye washabiki wengi nchini,ama siasa nyingi na majingambo mengi ambayo hayasaidii katika kujenga timu.
Musoti ni beki wa kimataifa na ana uwezo mkubwa sana katika ukabaji leo hii anaachwa na hatukuona nafasi yake anasajiliwa beki mzoefu kwa lengo la kuziba nafasi yake. Isihaka bado hajawa na uzoefu katika mikikimiki ya mechi mbalimbali, wadau wengi bado wanajiuliza maswali je ni kocha hakuridhika na kiwango cha mchezaji huyo ama kamati ya usajili kwa ajili ya kufurahisha mashabiki wake na uongozi mpya uliopo sasa?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni