SARE,ya tano mfululizo katika klabu ya Simba imewachanganya viongozi pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Phiri na benchi lake la ufundi, mpaka kufikia hatua ya kuwatuhumu baadhi ya wachezaji wa timu hiyo akiwemo Amri Kiemba na Haruna Chanongo kuwa hawajitumi ipasavyo.
Kwa kawaida matokea ya timu hiyo ni mazuri kwani mpaka sasa haijafungwa katika ligi ya Vodacom Tanzania Bara kufungwa,sare na kupata point ni moja ya matokeo ya mpira wa mguu kwa hali inavyoendelea. Kunaelekea katika timua timua ya kocha,wachezaji kutuhumiwa kuwa wanahujumu timu kwani ndio ilivyo katika klabu zetu kongwe hapa nchini zenye viongozi walioathirika kimawazo.
Tujiulize nani wa kulaumiwa katika timu hiyo kati ya wachezaji na kocha? ama uongozi wenyewe ukae chini ujiulize nani mchawi wa sare tano kwa upande wangu naona ndani ya uongozi kuna matatizo, kuna kundi la Ukawa ambalo limefutwa uanachama kuwa waliipeleka Simba Mahakamani katika kipindi cha Uchaguzi uliopita.
Kwanini nasema kuwa kuna matatizo katika timu hiyo ni kuwa baadhi ya wachezaji wameanza kutuhumiwa kuwa wanahujumu timu kwa mjibu wa kiongozi moja wa timu hiyo, amefikia hatua ya kusema katika chombo kimoja cha habari kuwa, Amri Ramadhani Kiemba anahujumu timu kwa kucheza chini ya kiwango akiwa kwenye timu ya Taifa Star anacheza kwa kujituma.?
Kweli kwa hali ilivyo Kiongozi kuanza kumtuhumu mchezaji kwa kuangalia kocha Phiri hampi nafasi kubwa ya kucheza na kwenye kikosi chake huku timu ya Taifa anaaminiwa na kocha mkuu. Sasa kiongozi huyo ana ushahidi gani kuwa mchezaji huyo anahujumu timu? basi angejaribu japo kutumia busara ya kuzungumza na wachezaji anaowahisi wanaihujumu timu kwanza au hata kundi linalijiita Ukawa pamoja na Baraza la Wazee wa timu hiyo ambao wanaonekana kutengwa na Uongozi na sio kuwanyoshea kidole wachezaji.
Huo unaonekana kuwa mwanzo tu lakini inawezekana zengwe hili litamkuta hata kocha mkuu wa wa timu hiyo kwani baada ya kutoka sare na Prison ya mkoani Mbeya kuna mambo mengi yatatokea katika timu likiwemo la kusimamishwa kwa wachezaji kumkalisha kitimoto kocha mkuu na benchi lake la ufundi. Kwa matokeo mabaya yanayoikumba klabu hiyo usije kushangaa kuona Kiemba,Shabani Kisinga na Haruna Chanongo wamesimamishwa kwa kutuhumiwa kwa kuhujumu timu.
Hivyo tunachoomba wana msimbazi waendelee kuwaamini wachezaji na sio kuanza kutuhumu kwa mambo ya siasa kwani tatizo wanalo wenyewe cha kuwashauri wakae chini na Ukawa na Wazee wa klabu hiyo, ili watatue matatizo ya timu na wala sio kuwalaumu wachezaji. Tunajua kuwa Simba ina Rais anayejua mpira Evans Aveva atumie busara kutatua mgogoro uliopo ndani ya timu maana inavyoelekea mambo yataendelea kuwa magumu kupita maelezo.
itaendelea wiki ijayo
MIKIKIMIKIKI
Uchambuzi,matokeo na Ratiba za mechi mbalimbali za mpira wa miguu
Jumatatu, 27 Oktoba 2014
Ijumaa, 24 Oktoba 2014
DUNIA ITASIMAMA KWA DAKIKA 90 USIKU WA EL CLASSICO
DUNIA itasimama kwa muda wa dakika tisini majira ya saa moja kamili usiku pale mahasimu wa soka nchini Hispania Barcelona na Real Madrid katika mechi ya la liga, upinzani uliopewa jina la El Classico na pia zikipambwa na majina makubwa ya wanasoka wenye upinzani mkubwa kwa soka la sasa Messi na Ronaldo.
Upinzani utaongezeka kwa pande zote mbili kwani kila timu imesajili wachezaji wapya, macho na masikio ni kwa nyota mpya wa timu ya Barcelona Luis Suerez, kwa mara ya kwanza ataonekana katika timu yake. Baada ya kumaliza kifungo cha miezi minne baada ya kumnga'ta mchezaji wa timu ya Taifa ya Italia la katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil.
Kwa upande wa mechi yenyewe itakuwa ngumu kwa kila upande kwani sasa timu ya Barcelona haijafungwa na pia haijaruhusu goli lolote katika michezo minane ya ligi hiyo na kujikusanyia point ishirini na mbili imeshinda saba na kutoka sare moja. Na mahasimu wao wana point kumi na nane wamefungwa mechi moja na kutoka sare moja.
Macho ya wengi ni kwa wachezaji wa timu hizo Lionel Mess, Christian Ronaldo ndio wanatazamwa kwa kila mtu kutokana na ubora walio nao kwa sasa japo kuwa Ronaldo anaongoza kwa kupachika magoli kwa ligi hiyo ana magoli kumi na tano na mpinzani wake ana magoli saba.
Je Luiz Suerez ataanza vyema kwa timu yake kwa kushirikiana na nyota aliye kwenye kiwango cha juu kwa sasa na ndie anaongoza kwa kupachika magoli katika klabu yake Junior Santos Nermar pingo kubwa litakuwa kwa Real Madrid kwa kumkosa winga wao hatari aliye majeruhi Gareth Bale.
Alhamisi, 23 Oktoba 2014
HATIMAYE REAL MADRID YALIPA KISASI CHA MWAKA 2008 KWA LIVERPOOL
KISASI timu ya Real Madrid toka nchini Hispania usiku wa kuamkia leo imetoka kifua mbele baada ya kulipa kisasi cha mwaka 2008 cha kufungwa magolin manne kwa moja mshambuliaji aliye kwenye kiwango cha Dunia Christian Ronaldo ameendelea kucheka na nyavu za wapinzani baada ya kufungwa goli la kwanza na magoli mawili yakifungwa na Karim Benzema yote yakipatikana kipindi cha kwanza.
Matokeo mengine Atletico Madridi wakiwaangamiza Malmo FC magoli matano kwa bila,huko nchini Uturuki vibonde Galatasaray wameendelea kugawa point baada ya kufungwa magoli manne kwa bila na vibonde wa ligi ya Ujerumani Borrusia Dotmund ambao mpaka sasa hawajafungwa goli lolote kwenye kundi hilo.
Arsenal wamepata ushindi wao kwa taabu baada ya kuwafunga Anderlecht magoli mawili kwa moja nchini Ufaransa Monaco wakitoka sare ya bila kufungana na Benfica huko kibibi kizee Juventus toka nchini Italia wakipokea kichapo toka kwa Olimpiakos kwa goli moja kwa bila.

MZUNGUKO ROUNDI YA TANO LIGI YA VODACOM TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII SIMBA NA YANGA UGENINI?
Mzunguko roundi ya tano wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara kuendelea tena mwishoni mwa wiki hii katika viwanja tofauti tofauti macho na masikio ya wengi yatakuwa katika viwanja vya Kambarage mjini Shinyanga na Sokoine mjini Mbeya huku vigogo vya Simba na Yanga vitakuwa ugenini.
Mechi nyingine mabingwa watetezi wa ligi hiyo Azam FC watakuwa nyumbani kuwaalika watoto waliokuwa usingizini Jkt Ruvu katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salamu huku watoto wa Mabati Pwani Ruvu shooting mara baada ya kuzinduka mpaka kupelekea kufukuzwa kwa kocha wa Ndanda FC watakuwa nyumbani kupepetana na Polisi Morogoro,wagonga nyundo Mbeya City baada ya kupokea kichapo toka kwa Azam watakuwa nyumbani kuwapokea vijana toka kwenye mashamba ya Miwa Mtibwa Sugar.
Je Simba atavunja mwiko dhidi ya Tanzania Prison katika uwanja wa Sokoine ambao umekuwa mgumu mno kwa wekundu wa msimbazi mara nyingi tumeshudia wakichezea vichapo ama kutoka sare Simba hawana bahati katika viwanja vya mikoani kwani hata msimu uliopita walipata point tatu tu katika mechi za ugenini nyingi walitoka sare pamoja na kufungwa ushindi wao ulikuwa katka uwanja wa Sheik Abedi Karume mjijini Arusha dhidi ya Jkt Oljoro.
Watoto wa Marcio Maximo watakuwa wageni wa timu mpya iliyo panda ligi kuu kwa mara ya kwanza Stand United ambayo mpaka sasa haijapoteza mechi yeyote ya ugenini kwani imeweza kupata pointi tano japo ilianza vibaya katika uwanja wake wa nyumbani kwa kufungwa magoli manne kwa moja na Ndanda FC,je watakuwa wateja katika uwanja wake dhidi ya timu ya Yanga?
Mara nyingi tumeshudia timu za Simba na Yanga zinapocheza ugenini huwa zinakabiwa mno na timu pinzani kutokana na kuwa na majina makubwa katika soka la Tanzania mambo mengi hutokea katika mechi hizo ushirikina mara nyingi hutokea mfano msimu uliopita mjini Tanga mchezo baina Jkt Mgambo naTimu ya Yanga na Mbeya City na Simba mjini Mbeya mambo hayo ya ushirikina yalitokea katika viwanja vingi ambapo Simba na Yanga zinapokuwa ugenini.
Kwa muda mrefu wakazi wa mjini Shinyanga hawakuwa na timu kwa takribani miaka kumi hawazioni timu za Simba naYanga baada ya timu yao iliposhuka daranja Kahama Unitedi hajawahi tena kuona uwanja wao ukitumika tunajua jumamosi mechi itakuwa kali na kusisimu kwa timu zote mbili na pia uwanja utafurika mno hii kutokana na watu wengi wa kanda ya ziwa kuwa hamasa ya mpira.
Hivyo tunatarajia kuwa mechi yote itakuwa migumu kutokana na kila timu zimejipanga vya kutosha katika safari ya kutafuta pointi tatu muhimu kwa kila timu wasimamzi,wamzi tunawaomba wafate sheria zote za mpira wa miguu hatutaki kuona wakipendelea timu fulani pamoja na timu zitakapofungwa mara nyingi tumeona makocha huwa wanalalamika pindi timu zinapofungwa utasikia refa kapendelea timu fulani ama viwanja vibovu yote hayo hutokea mara tu dakika tisini za mwamuzi zinapoisha.
Jumatano, 22 Oktoba 2014
JE LIVERPOOL KUENDELEZA UTEJA KWA REAL MADRID AU REAL MADRID KULIPA KISASI LEO HII?
USIKU wa ulaya kuendelea leo hii katika viwanja tofauti tofauti swali la kujiuliza nani atavuna idadi kubwa ya magoli kama mechi za jana kwani magoli 40 yalipatikana huku Bayern Munich na Shakhtar Donestik zikifanya mauaji ya kutosha kwani ziliweza kushinda kwa idadi kubwa ya magoli.
Macho na masikio yatakuwa nchini England majogoo wa Anfield Liverpool watakuwa wanapepetana na mabingwa watetezi wa kombe hilo Real Madrid toka Hispania huo utakuwa mchezo mkali na wa kuvutia kwa timu zote mbili kwani zinapokutana huwa zina upinzani mkubwa mno.
Je Liverpool wataendeleza ubabe kwa mabingwa hao ama Madrid watalipa kisasi cha magoli manne waliofungwa katika mechi ya mwisho kukutana mwaka 2008\09 katika mchezo wa kwanza Liverpool alishinda goli moja kwa bila na ziliporejeana kwa mara nyingine Liverpool alishinda magoli manne kwa moja.
Mechi nyingine watoto wa kaskazini mwa London timu ya Arsenal watakuwa ugenini nchini Ubelgiji kupepetana na Anderlecht,Nchini Ufaransa matajiri Monaco wanaochechemea katika ligi ya kwao watawapokea vijana toka Ureno Benfica, vibonde toka Ujerumani Borrusia Dotmund watakuwa ugenini na wahuni wa Uturuki Galastaray,Atletico Madrid watakuwa nyumbani na Malmo FC.
Jumatatu, 6 Oktoba 2014
LIGI ya Vodacom Tanzania bara ipo katika mzunguko wa tatu tumeshudia timu mbalimbali zikiendeleza ushindi nyingine sare pamoja na kufungwa hayo yote ni matokeo ya mpira kwani kuna kushinda,sare na kufungwa.
Je tutafika katika kukuza mpira wa Tanzania tuwe kama nchi nyingine barani Afrika ama Ulaya? kwani mpaka sasa kuna mvutano baina ya TFF na timu zinazoshiriki katika ligi hiyo shirikisho linalosimamia mpira tayari limesema lazima kila timu ikatwe asilimia tano ya wadhamini wa ligi.
Ambao ni Vodacom pamoja na Azam Media kwani ndio wadhamini wa ligi hiyo kwa mjibu wa TFF wamesema wameazisha mfuko wa maendeleo ya timu za vijana na mapato yake yatapatikana kutokana na makato ya vilabu vinavyoshiriki ligi ya Vodacom je huu ni mfumo sahihi kwa shirikisho hilo chini ya Rais Jamal Malinzi vimezingatia hali halisi iliyopo katika timu zinazoungaunga kupata hela?
Kuna haja gani vilabu vikatwe mapato kama hayo kwanini TFF isibuni njia nyingine ya kupata hizo pesa za kuendeshea vijana mpaka isake mapato kwa timu hizo huu ni mgogoro mkubwa mno kwani kila upande ukimtunishia misuri mwenzake na tayari Malinzi kasema lazima kila timu ikatwe asilimia tano huku mwanasheria wa vilabu hivyo Damasi Ndumbaro amesema haiwezekani kukatwa asilimia hiyo.
Je timu kama Stand United ,Ndanda Fc, Coast Union, ambazo zinapata hela kutoka kwa kutembeza bakuli kwa watu zitaweza kweli kuwalipa mishahara wachezaji na benchi zima la ufundi mpaka leo hii vilabu vinalia pesa haitoshi kwa mahitaji ya timu haki imetendeka ama shirikisho hilo limekurupuka kwa maamuzi hayo kwa vilabu.
Kwa hili naona TFF hawajatenda haki kwa kuamua kuingia kwenye mvutano ambao hauna maana kwa kuendesha mpira wa miguu wangebuni kitu kingine cha kuwaingizia mapato bila wasiwasi mfano mzuri wangeandaa semina kwa wadau wa mpira na pia wangeandaa mechi maalum kwa timu ya Taifa kwa lengo kupata hizo pesa na pia wangetafuta wadhamini.
Kwa ushauri wangu kwa shirikisho hilo liache kutumia nguvu kwa vilabu hivyo bali litumie vyanzo vingine kwa kuendeshea mfuko huu ambao wameanzisha na sio kwa kuzizamisha timu mpaka ikapelekea kuvurungika kwa ligi hiyo, maana tunapoelekea mambo mengi yataendelea kutokea.
Hivyo busara itumike kwa maamuzi hayo hatupendi kuona soka letu likiendelea kuwa chini badala ya kufikiri mbele kwani sisi tunazozana na makato ya pesa wenzetu wanafikiria maandalizi ya kombe la Dunia mwaka 2018 litakalo fanyika nchini Urusi.

Jumamosi, 4 Oktoba 2014
MASIKINI SIMBA AKOSA NYAMA KAOKOTEZA MAJANI
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara imeendelea tena wikiendi hii huku michezo kadhaa ikipigwa katika viwanja vitano tofauti lakini kubwa zaidi ni ile mechi kati ya Simba na Stand United iliyochezwa uwanja wa taifa Dar Es Salaam ikishuhudiwa Simba ikilazimishwa tena sare ya goli moja kwa moja.
Hii ni sare ya tatu kwa timu ya Simba tangu ligi kuu ianze na hivyo imepata pointi tatu na magoli manne katika michezo mitatu walioicheza tena katika uwanja mmoja wa taifa, hali inayoonesha kuwa bado haijajipanga vizuri kukabiliana na mikikimikiki ya ligi kuu inayoonekana kuwa ngumu kwa timu zote kucheza kwa juhudi kuhakikisha wanavuna pointi tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania kombe hilo.
Kuna mambo ambayo huibuka pindi hizi timu kongwe kama Simba inapozidiwa na kutoa matokeo ya aina kama hii kuwa inawezekana kuna tatizo, huku wakisahau kuwa mchezo ni mabadiliko na kila timu inafanya jitihada kubwa kuhakikisha inavuna pointi tatu. Hivyo matokeo wanayoyapata ni ya kawaida sana kutokana na ukweli kuwa kwa sasa dunia imebadilika na kila timu imebadilika na inafanya kila mbinu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Hivyo ni bora wapenzi na wadau wa soka wakaelewa kuwa mpira hausimami katika umbo lilelile bali hubadilika kulingana na wakati na namna dunia inavyoendelea, kinachotakiwa kwa timu ya simba ni kuhakikisha wanabaini nini kinawakwamisha kupata ushindi ili kujikwamnua na hali hii inayoonekana kuwakatisha tamaa mashabiki wa timu hiyo

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)